
Jedwali la ligi ya EPL limeanza kutenganisha farasi, punda na vihongwe katika mbio za ubingwa baada ya kila timu kushiriki mechi 9.
Manchester United imekuwa timu ambayo imeanza msimu vibaya, mpaka sasa ikiwa imeshikilia nafasi ya 14 kwenye jedwali.
Hata hivyo, imebainika kwamba Man Utd licha ya kukaribia kuburuta mkia kwenye msimamo wa ligi, kwa upande mwingine inashikilia kidedea kwa timu zilizopoteza nafasi nyingi za mabao.
Kulingana na takwimu zilizoachiliwa na premier league baada ya kukamilika kwa mzunguko wa raundi ya 9 ambapo Man Utd ilititigwa na West Ham 2-1, klabu hiyo imepoteza jumla ya nafasi 22 za wazi kufunga mabao.
Tottenhma pia wamepoteza nafasi 22 za wazi huku Arsenal na Brentford wakifuata kwa ukaribu katika orodha hiyo kwa kupoteza nafasi 20 za wazi kila mmoja.
Bruno Fernandes, Joshua Zirkzee na Alejandro Garnacho ndio wachezaji ambao wamepoteza nafasi nyingi zaidi kwa timu.
Marcus Rashford, kwa upande wake, amekuwa akifanya vyema mbele ya goli hadi sasa msimu huu.
Kwa ujumla, Man United wana pointi 11 kutoka kwa mechi 9, ikiwa ni rekodi mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika klabu hiyo katika miaka ya hivi karibuni.
Matokeo yao dhidi ya West Ham yameibua tena mjadala kuhusu uhakika wa meneja Erik Ten Hag kuendelea kusalia usukani kama mkufunzi wao, huku wakijiandaa kukaribisha Chelsea wikendi ijayo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!