Timu ya taifa, Harambee Stars, imepata pigo kubwa baada ya kiungo wa kutegemewa Kenneth Muguna kupata jeraha saa chache kabla ya mechi muhimu ya kufuzu kwa Chan 2025 dhidi ya Sudan Kusini.

Shirikisho la Soka la Kenya lilithibitisha habari hiyo kupitia taarifa rasmi, ikionyesha kwamba mchezaji huyo mwenye uzoefu ambaye anachezea Kenya Police katika Ligi Kuu ya Kenya hangeweza kusafiri na kikosi hadi Juba.

“Kiungo Kenneth Muguna ameondolewa kwenye kikosi baada ya kufeli mtihani wa utimamu wa mwili,” Shirikisho lilitangaza.

Kocha mkuu wa Harambee Stars Engin Firat amemwita mchezaji wa Nairobi City Stars Clifford Otieno kuziba nafasi iliyoachwa na Muguna.

Timu hiyo iliondoka Ijumaa kuelekea Sudan Kusini kwa mechi ya mkondo wa kwanza itakayochezwa Jumapili kwenye uwanja wa taifa mjini Juba.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mechi ya mkondo wa pili imepangwa Jumapili, Novemba 3 kwenye uwanja wa Mandela Taiafa huko Nambole, Uganda.