Ni Mwamko mpya kwa waunda maudhui na wapenzi wa upigaji picha kwa simu.  Kampuni ya Vivo imeshirikiana na ZEISS kuzindua simu yenye uweledi wa kupiga picha bora.

Meneja wa mawasiliano wa Vivo Kenya James Irungu alisema uzinduzi wa simu ya V:vivo 40 unaanzisha mwamko mpya katika teknojia ya upigaji picha za ustadi wa juu kwa waunda maudhui na wenye nia ya kutayarisha makala aina mbali mbali.

Mafanikio haya yanatokana na ushirikiano wa karibu katia ya kampuni ya Pioneer ZEISS na Vivo na umepelekea kuzinduliwa kwa aina mpya ya simu ya V - V40. Simu hii mpya inaleta mwamko mpya wa upigaji picha wa simu kupitia mfumo wa upigaji picha uliobuniwa kwa pamoja na ZEISS, kampuni inayoongoza kimataifa katika nyanja ya upigaji picha yenye zaidi ya miaka 177 ya uzoefu usio na kifani.

Ushirikiano huu unaleta utaalam wa ZEISS wa upigaji picha kwenye V40, na kuahidi hali ya upigaji picha za  ustadi kwa kiwango cha juu kwa watumiaji.

Kulingana na Iringu ZEISS imekuwa ikitengeneza teknolojia za hali ya juu zaidi za kupiga picha, baadhi zikiwa ni mafanikio ya upigaji picha na sinema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Ushirikiano kati ya vivo na ZEISS umeleta mfumo bora wa kupiga picha kwa vivo V40, ili kuwawezesha watumiaji kunasa taswira za hali ya juu kwa ustaarabu. Kamera kuu ya ZEISS All Main inaleta uboreshaji wa mwonekano na hisia za sinema za kiwango cha juu mfukoni mwako. 

Vivo V40 ni ya hivi punde zaidi, iliyoundwa kwa ushirikiano na ZEISS, ni mfano wa harakati za vivo za upigaji picha za kitaalamu. vivo inazidi kuinua kiwango cha upigaji picha mahiri kwa simu, ikilenga kumpa kila mtumiaji ubora wa sinema kwa uundaji wa kibinafsi na kujieleza katika enzi ya upigaji picha wa vifaa vya mkononi. V40 inajumuisha kipengele cha Video ya Sinema ya ZEISS ili kuinua hali ya utumiaji wa video ya rununu ya watumiaji hadi viwango vipya.

Kwa ZEISS Focus Transition na ZEISS Cinematic Video Bokeh, watumiaji wanaweza kutarajia kunasa video za kiwango cha kitaalamu zenye madoido ya ajabu ya bokeh na mabadiliko laini ya umakini kwa urahisi.  

Zaidi ya hayo V40 imewekwa kuanzisha AI 3D Studio Lighting, kipengele ambacho kinatumia algoriti za hali ya juu za AI kwa utambuzi wa mwanga  wa 3D. Teknolojia hii huongeza mwangaza katika mazingira ya gizai.

vivo V40 itabadilisha jinsi unavyorekodi maisha, kuwezesha kila mtu kuwa mwelekezi wa hadithi yake mwenyewe.