Wanawake watatu wenye umri wa makamo walifikishwa katika mahakama ya Eldoret wakishtakiwa kwa kumdhulumu mwakamke waliyedai anachepuka na wanaume wao.

Kwa mujibu wa kesi hiyo, wanawake hao walimuadhibu mwanamke huyo kwa kumuingiza pilipili katika uke wake, wakisema kuwa hilo lingekuwa funzo dhidi ya kuchepuke na wanaume wa wenyewe.

Mwathiriwa, mwenye umri wa miaka 24, alipata majeraha kwenye sehemu zake za siri wakati wa shambulio hilo.

Walishtakiwa kwa kosa la unyanyasaji wa kijinsia kinyume na makosa ya ngono ya 2007.

Pia walikabiliwa na shtaka la pili la unyanyasaji.

Watatu hao walikanusha mashtaka walipofika mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Eldoret na Mahakama iliagiza waachiliwe kwa dhamana ya pesa taslimu Sh100,000 kila mmoja.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 4, 2024.

Polisi wanasema washukiwa hao walimkandamiza mwathiriwa alipokuwa akielekea soko la mtaani na kumfanyia shambulio la kinyama kwa kumuwekea pilipili sehemu zake za siri huku wakimtaja kama mnyakuzi wa wanaume.

Inadaiwa kuwa kisa hicho kilitokea katika soko la Kapseret katika Kaunti ya Uasin Gishu mnamo Oktoba 1, 2024.

Mwathiriwa alikuwa amelalamika kwa polisi na kupelekea kukamatwa kwa watatu hao