KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Septemba 24.
Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Bungoma, na Kisii.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Muthaiga na Mukuru Kwa Njenga zitaathirika na kukatizwa kwa umemem kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Mulaku na Karima katika kaunti ya Bungoma zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Marani na Sombogo katika kaunti ya Kisii pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!