
Katika klipu ya video ambayo imekuwa ikienezwa kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa hafla ya mazishi ya kijana huyo yaliyofanyika Jumatano katika kaunti ya Kiambu, baadhi ya wanafamilia walionekana wakizungumza kwa hasira na ghadhabu kuhusu kutengwa katika matumizi ya hela zilizochangwa kwa ajili ya kumpa buriani Mwangi.
“Hatukufurahia, sisi kama familia Gerald angekufa bila nyinyi kumjua tungemzika. Lakini vile tunamzika hivi hatuna raha kabisa, hata pale tunampumzisha sijui tunampumzisha vipi,” alisema mwanafamilia mmoja.
“Jana mama ameenda kufuatilia kama kila kitu kiko sawa. Jeneza tulikuwa tumepigiwa picha wakisema watanunua, mamake hakuitwa kuenda kununua jeneza, na kitu kingine hatujawahi kutumiwa hata shilingi na hatujawhai uliza. Kama kuna watu wako kwenye kikundi wanajua inatuuma sana sisi kama familia hatujashindwa na kuzika Gerald. Tulikuwa tayari sisi lakini tukawakabidhi marafiki zake, sasa kwa nini mnatufanyia hivi tuliwakosea nini?” alihoji zaidi kwa majonzi.
Mwanafamilia huyo alizama zaidi akidai kwamba mzazi wa Gerald alitaka kujitoa uhai kutokana na kile kilichokuwa kikiendelea kwenye kikundi cha mtandaoni na kutaka kama hawatomheshimu basi wamheshimu marehemu.
Marehemu Gerald Mwangi alifariki wiki mbili zilizopita baada ya kile kilichotajwa kuwa ni kuhusika katika ajali na baadae kupoteza maisha akipokea matibabu hospitalini.
Mwangi, aliyekuwa anafahamika kama Makanga Bae kutokana na utanashati wake alikuwa ni mhudumu katika kampuni moja ya magari ya uchukuzi wa umma jijini Nairobi.
Alijizolea umaarufu kutokana na jinsi alikuwa anaweka ndefu zake za kuvutia kwa wengi, haswa watoto wa kike ambao walimpa jina la utani kuwa ‘Makanga Bae’.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!