Wakili Donald Kipkorir amemtetea vikali wakili mkongwe John Khaminwa baada ya kuonekana kurushiana cheche za maneno na aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali, Githu Muigai.
Khaminwa na Muigai walikutana katika mahakama ya Milamani Jumanne alasiri wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya kupinga kubanduliwa ofisini kwa Rigathi Gachagua kama naibu rais.
Khaminwa, 88, ambaye amehudumu kama wakili kwa zaidi ya miaka 54 alikuwa akimtetea Gachagua dhidi ya kubanduliwa kwake huku Githu Muigai akiwa upande wa bunge.
Muigai alilenga kuzungumza mbele ya Khaminwa kwa kigezo kwamba yeye ni mwanasheria mkuu lakini Khaminwa akakataa kukubali hilo akimkumbusha kwamba wakati anaanza kuhudumu kama wakili, yeye [Muigai] bado alikuwa ananyonya.
Ni kutokana na cheche hizi za maneno ambapo Wakenya kwenye mitandao ya kijamii walionekana kuchukua kila mmoja upande vwake, wengi wakionekana kumsuta Muigai kwa kutomheshimu Khaminwa mahakamani licha ya kuwa anamshinda umri mara dufu.
Mmoja wa walioonyesha msimamo huo ni wakili Donald Kipkorir ambaye alisema kwamba hakuna mwanasheria yeyte vanayeweza kumzidi Khaminwa katika utekelezaji wa sheria na kesi za mahakamani humu nchini.
“Dk. John Khaminwa amekuwa mwanasheria thabiti zaidi nchini Kenya katika utendaji wake wote wa sheria. Daima amesimama kwa Utawala wa Sheria na Katiba. Hajawahi kusaliti imani yake kwa pesa. Ametoa dhabihu kazi yake na pesa zake kwa ajili ya kuwakilisha watu ambao Mfumo wa siku ule ulifikiriwa kuwa Wapotoshaji,” Kipkorir alimpa maua yake.
“Hakuna wakili mwingine nchini Kenya anayeweza kushikilia mshumaa juu ya Khaminwa. Khaminwa anasimama juu ya mawakili wote nchini Kenya. Kutomheshimu Khaminwa ni uthibitisho wa kutotosheleza. Khaminwa hajawahi kutafuta upendeleo wa kisiasa kutekeleza sheria. Khaminwa ndiye mwanasheria pekee anayewakilisha yote yanayomwendea bila kujali kabila, Imani, jinsia au ushawishi wa kisiasa. Anakaa juu ya Mazoezi ya Kisheria bila rika!” alimsaifia zaidi.
Kesi hiyo ya kupinga kubanduliwa kwa Gachagua itaendelea tena leo hii.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!