Mwaka huu umeshuhudia watu mashuhuri kadhaa wa Kenya wakiwemo wanamuziki, waigizaji, wanahabari na waundaji wa maudhui wakiwapoteza wazazi wao.

Hivi majuzi, aliyekuwa mchekeshaji wa Churchill Show Mannerson Oduor almaarufu Akuku Danger alimpoteza baba yake mzazi ambaye alifariki kutokana na saratani.

Mchekeshaji na mtangazaji wa redio David Oyando almaarufu Mulamwah pia alimzika mama yake mlezi baada ya kumpoteza mapema mwezi huu.

Hii hapa orodha ya mastaa wengine wa Kenya waliofiwa na wazazi wao;-

• Akuku Danger (Mchekeshaji) - alimpoteza babake, Oktoba 2024

• Mulamwah (Mchekeshaji) -alimpoteza mama mlezi, Oktoba 2024

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

• Mr Lenny (mwimbaji mkongwe) - alimpoteza baba, Septemba 2024

• Mashirima Kapombe (Mwanahabari) - alimpoteza mamake, Septemba 2024

• Frasha (Rapa mkongwe) - alimpoteza baba, Agosti 2024

• Mr Seed (Mwimbaji) - alimpoteza mamake, Agosti 2024 • Patricia Kihoro (Mwanahabari) - alimpoteza babake, Julai 2024

• Nicki Bigfish (Mtayarishaji Maudhui) - alimpoteza babake Februari 2024