Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Kalerwa Salasya mnamo siku ya Jumanne alizungumza kwa utani kuhusu ziara yake ya kikazi katika kaunti za Bomet, Kisii na Nyamira ambapo yeye na kamati ya bunge ya kilimo walikuwa wameenda kutafuta suluhu kwa wakulima wa majani chai.
Katika chapisho ambalo aliweka kwenye mitandao ya kijamii, mwanasiasa huyo kijana alishiriki picha iliyoonyesha akiwa kwenye mazungumzo na mbunge wa kuteuliwa Sabina Wanjiru Chege.
Salasya alieleza kuwa yeye na Bi Chege wanahudumu katika kamati moja bungeni na walikuwa wameenda kufuatilia masuala ya ukulima wa majani chai.
“Sabina, ni mwenzangu katika kamati ya kilimo katika kamati ya kilimo katika bunge la kitaifa. Kwa sasa niko naye katika ziara yetu ya Bomet, Nyamira, na Kisii katika kutafuta suluhisho la wakulima wa chai,” Salasya aliandika.
Katika chapisho hilo, pia alizungumza kuhusu msimamo wake kuhusu kuwa katika uhusiano na wanawake wenye umri mkubwa. Alibainisha kuwa asingependa kuingia katika vishawishi vya kutoka kimapenzi na wanawake wakubwa, maarufu kwa jina la ‘wamama’ kwani amesikia si rahisi kujiondoa.
"Roho ya kupenda wamama isiwahi kunifwata nasikianga wanajua kulinda vijana wadogo kama mimi hadi wanajisahau," alisema.
Haya yanajiri wiki chache tu baada ya mbunge huyo kwa mara ya kwanza kujaribu kumteka sosholaiti maarufu wa Kenya Huddah Monroe.
Baada ya wiki nyingi za kumfuatilia kwa dhati mwanasosholaiti Huddah Monroe, mwezi uliopita Salasya alitangaza kuwa hataki tena kufanya hivyo.
Katika ujumbe wake, Mbunge huyo wa Mumias Mashariki alidai kwamba juhudi zilizohitajika kumchumbia mrembo huyo ni nyingi mno. Pia aliomba msamaha kwa wasichana wa 'kienyeji' kwa kuwaacha kutafuta malisho ya kijani kibichi.
“Hawa wanaotaka pesa sina uwezo wataishusha Serikali yangu ngoja nirudi kwenye kienyeji wangu, najitenga rasmi na huyu kifaranga, maoni yoyote niliyotoa ambayo yalimuumiza kienyeji changu chochote nje hapa naomba mnisamehe ilikuwa tu mambo ya mitandao ya kijamii. Mnisamehe nyinyi ndio munawezana na mimi huyu mtu wash wash ndio wako na pesa ya uponyaji,” alisema.
Mbunge huyo alikuwa na misheni kwa muda wa miezi miwili ya kuhakikisha anatafuta njia za kuwavutia Huddah, ili hatimaye wachumbiane naye.
Tamaa yake ilimwona akitoa jumbe nyingi za mapenzi yake kwa msosholaiti huyo, na pia kumnunulia maua.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!