Jumatatu, Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ilimuagiza Naibu Rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua kurekodi taarifa kuhusu madai kuwa kumekuwa na majaribio ya kumuua.

Hayo yalikuwa baadhi tu ya madai mazito ambayo naibu rais huyo wa zamani alitoa dhidi ya rais William Ruto na serikali ya Kenya. Gchagua alizungumza baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini mnamo Oktoba 20.

Madai ya Gachagua ni pamoja na:

* Kupunguzwa kwa maafisa wa usalama.

* Kuondolewa kwa magari ya serikali.

* Kutumwa nyumbani kwa wafanyakazi 108.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

* Majaribio mawili ya mauaji.

* Kasi ya mchakato wa kuondolewa ofisini.

* Kunyanyaswa sana katika mwaka mmoja uliopita.

* Kuzuiwa kuhudhuria Sherehe za Mashujaa, Kwale.

* Kutumiwa kushinda urais.