KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Oktoba 23.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kakamega, na Busia.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Muthaiga na Loresho zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za eneo la Shimanyiro katika kaunti ya Kakamega zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za mji wa Busia katika kaunti ya Busia pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!