
Wechuli, chifu maarufu kwa kauli ya ‘Misheveve na Sarat’ alikaribishwa bungeni na mbunge wake Caleb Amisi wa eneobunge la Saboti, kaunti ya Trans Nzoia.
Chifu huyo alielezea waandishi wa habari miaka ya nyuma jinsi mzozo ulivyoibuka baina na wanafamilia katika eneo lake kupelekea mfarakano, na jinsi alivyoelezea iliwapunga wengi.
Wiki chache zilizopita, watumizi wa mitandao ya kijamii walifufua kauli hiyo na kuifanya kuenea mitandaoni hivyo kumuibua tena kwenye jicho la wanamitandao.
Chifu huyo baada ya kufika Nairobi, alimtembelea mbunge Caleb Amisi kwenye ofisi yake katika majengo ya bunge.
Amisi alifichua kwamba chifu huy alimuelezea matatizo mbalimbali yanayowakumba wananchi wa eneo lake na pia wakatathmini njia ainati jinsi ya kudumisha usalama katika eneo hilo.
“Leo, nilimkaribisha chifu wa lokesheni ya Saboti katika Eneo Bunge la Saboti. Aliwasilisha masuala mbalimbali ya watu wa eneo la Saboti ofisini kwangu na kujadili njia za kuboresha usalama na ustawi wa wapiga kura wangu,” Amisi alisema.
“Ninakaribisha namna yake ya kuchekesha na ya kufurahisha ya kuwashughulikia raia na kushiriki njia za kimaendeleo zaidi za njia zisizo za mabishano za kudumisha sheria na utulivu katika jamii zetu za vijijini,” aliongeza Amisi.
Katika simulizi yake, chifu wa Misheveve alizungumza kuhusu mtu ambaye alishukiwa kumuua babake na kumshambulia mamake kufuatia mzozo wa kinyumbani kuhusu chakula.
Mshukiwa alikasirika kwamba mama yake alikuwa amepika majani ya maboga [misheveve] badala ya mboga yake aipendayo - sarat, na hivyo akamshukia mwanamke huyo kwa makofi na mateke.
Babake mshukiwa ambaye alikuwa ndani ya chumba chake wakati wa vurugu hizo alipaza sauti yake na mama huyo akatumia nafasi hiyo kukimbia.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!