KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, September 22.
Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Bungoma, Kakamega, na Kitui.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Muthiga, Roysambu, Zimmerman na Githurai 45 zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Sipala na Lwile katika kaunti ya Bungoma yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za eneo la Butere katika kaunti ya Kakamega zitakosa umeme kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Museve katika kaunti ya Kitui pia litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!