Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


Mwanasosholaiti na mfanyibiashara Huddah Monroe amedai kwamba nchini Kenya, hakuna siku utashuhudia cwatu kutoka jamii ya Mlima Kenya wakijitokeza kuandamanakisa kiongozi kutoka eneo hilo kadhulumiwa.

Akichapisha kupitia Instagram, Monroe alisema kwamba hakuna mtu hata mmoja kutoka Mt Kenya ajafanya uthubutu wa kuandamana barabarani au mitaani kisa naibu rais Rigathi Gachagua amebanduliwa.

Mrembo huyo alitetea msimamo huo akisema kwamba watu kutoka eneo hilo wana akili za kutosha na kusema iwapo hiyo ilikuwa njama ya rais Ruto kuona maandamano katika eneo hilo, basi ameula wa chuya.

"Watu walidhani watu wa murima wataenda barabarani kuandamana kwa sababu ya Gachagua. Akili nayo tulipewa rafiki yangu," Huddah alichapisha.

"Kama Ruto alifikiria atawasambaratisha Wakikuyu kuingia kwa mzozo kwa sababu ya Gachagua, pole sana, maono yetu ni makubwa kuliko siasa duni," Huddah aliongeza.

Kauli ya Huddah inajiri siku chache tu baada ya Rigathi Gachagua kubanduliwa kutoka ofisini na bunge la seneti katika kikao ambacho kiliendeshwa bila ya uwepo wake.

Mawakili wa Gachagua walisema kwamba alikuwa hospitalini na baada ya kutoka Hospitalini Oktoba 20, kiongozi huyo aliyebanduliwa alihutubia wanahabari nje ya hospitali ya Karen na kutupa cheche za maneno kwa aliyekuwa bosi wake, Rais William Ruto.

Gachagua alidai kwamba alipokonywa walinzi wake wote pamoja pia na wafanyikazi katika ofisi yake ya Harambee Annex kushrutishwa kuchukua likizo ya lazima.