Mwanaharakati maarufu wa kisiasa na wakili David Morara Kebaso alikumbana na kizingiti katika ziara yake ya Siku ya Mashujaa katika  kaunti ya Narok baada ya watu wasiojulikana kudaiwa kuwashambulia.

Kulingana na kiongozi huyo wa chama cha INJECT, mwanasiasa mkubwa wa Narok ambaye jina lake halikutajwa alituma wahuni kumshambulia yeye na timu yake mnamo siku ya Jumamosi walipokuwa wakizuru kaunti hiyo.

Morara alisema kuwa zaidi ya washambuliaji 50 walitumwa kwao na mwanasiasa huyo ambaye hakutajwa jina kwa lengo la kumzuia kufichua ukweli.

"Walipotoroka watu zaidi ya 50 ambao ulikuwa umewakodi kuziba barabara, majambazi wako walitufuata kwa magari mawili (prado na pickup nyeupe) na wanaweza kuonekana wakitushambulia," Morara alisema chini ya video ya shambulio hilo ambayo alichapisha.

Wakili huyo aliendelea kudai kuwa baadhi ya wanachama wa timu yake walikamatwa na kupigwa baada ya tairi la gari lao kupasuka.

“Tairi la gari letu lilipopasuka na lingine kuondoka barabarani, Wakenya hawa wasio na hatia walitelekeza magari hayo na kukimbia kwa miguu, walionaswa walipigwa katika jaribio la kuwaua. Haina mambo baba, leo ni sisi kesho ni wewe. Kwa watu wa Narok, nawapenda nyote. Utuombee. Msijali, naamini itabadilika,” alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika chapisho jingine, alionyesha picha za kichwa cha mtafiti wake Bw Mudhune ambaye alionekana kupaa majeraha wakati wa shambulio hilo.

Hapo awali, mwanaharakati huyo wa kisiasa kijana alikuwa ameomba usaidizi akidai kuwa baadhi ya watu wake wamejeruhiwa.

“Siwezi kuwasiliana na yeyote anayeweza kuwasiliana na polisi kufika kwenye lami kutoka Olulunga hadi Mau. Tafadhali,” Morara alisema katika chapisho moja.

Katika chapisho lingine, alisema, “Ninahitaji usaidizi niko Narok kwa sasa baadhi ya watu wangu wamejeruhiwa katika eneo la Ololulunga, Narok. Tafadhali saidieni wamejeruhiwa.”

Kwa muda wa miezi michache iliyopita, mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa akivuma kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari huku akihusishwa pakubwa katika kukosoa serikali ya kitaifa na kaunti.