Aliyekuwa
waziri wa Afya Susan Nakhumicha amefunguka kuhusu changamoto zilizofuata baada
ya kupoteza nafasi yake ya uwaziri miezi michache iliyopita.
Akizungumza wakati wa mazishi ya Bi Kukhu Rodah Lusaka, mamake gavana wa Bungoma Ken Lusaka, mnamo siku ya Ijumaa, Oktoba 18, waziri huyo wa zamani alibainisha kuwa si rahisi kurejea kuwa raia wa kawaida baada ya kushikilia afisi hiyo kubwa ya umma.
Kufuatia hayo, Nakhumicha alitoa ombi la dhati kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana la Kenya, Jackson Ole Sapit kumwombea huku akitumai siku njema zijazo.
"Unalala CS, hauamki ukiwa mmoja; unalala naibu wa rais, hauamki ukiwa mmoja. Tunamwachia Mungu kila kitu," Nakhumicha alisema.
Aliongeza, “Askofu, niombee. Si rahisi, umekuwa waziri, alafu ghafla, wewe ni Nakhumicha tu. Unajua jina langu ni la kipekee; ukitaja wengi wanajua ni waziri wa Afya. Niombee.”
Mnamo
mwezi Julai, Rais William Ruto alivunja baraza lake la mawaziri kwa jumla na
kumbakisha tu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi.
Ruto
aliwatuma nyumbani Mawaziri wote akiwemo Nakhumicha na Mwanasheria Mkuu
Justin Muturi.
Wakati
wa tangazo lake la Julai 11, Mkuu wa Nchi alisema baraza jipya la mawaziri lingetajwa
baada ya mashauriano ya kina katika sekta zote.
Aliongeza
kuwa mawaziri wote wakiwa nje ya afisi, maafisa wa uhasibu wa wizara miongoni
mwa maafisa wengine wangesimamia utendakazi.
"Nimeamua
kuwafuta kazi mara moja makatibu wote wa baraza la mawaziri na mwanasheria mkuu
wa Baraza la Mawaziri la Kenya isipokuwa Waziri Mkuu wa Baraza la Mawaziri na
Waziri wa Masuala ya Kigeni," Ruto alisema.
Siku chache baadaye, rais alitaja baraza lake jipya la mawaziri akiwakumbuka mawaziri kadhaa ambao alikuwa amewafuta kazi lakini akawaacha baadhi yao wakiwemo Susan Nakhumicha, Peninah Malonza, Zacharia Njeru, Ezekiel Machogu, Ababu Namwamba, Mithika Linturi, Florence Bore, Eliud Owalo, Simon Chelugui, Aisha. Jumwa na Njuguna Ndungu.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!