Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru ameandika ujumbe wa pongezi kwa waziri wa mambo ya ndani Kindiki Kithure.
Haya yanajiri huku kukiwa na ripoti kuwa seneta huyo wa zamani wa Tharaka Nithi ndiye naibu wa rais ajaye.
Huku akimpongeza, Waiguru alimsifu profesa huyo wa sheria na kumshauri amsaidie rais William Ruto katika kutawala nchi vyema.
“Ndugu yangu Profesa Kindiki Kithure, pongezi zangu za dhati. Kwako wewe historia imeweka heshima na wajibu unaotolewa kwa wachache tu. Mungu akuongoze wewe na HE William Ruto unapoongoza nchi hii kuu kufikia uwezo wake mkubwa,” Waiguru alisema kwenye taarifa.
Gavana huyo aliendelea kuwashukuru waliompendekeza kushika nafasi hiyo.
“Kwa wale walioniunga mkono kwa nafasi hii, nawashukuru. Ni lazima sasa tujitolee juhudi zetu za kujenga Kenya bora chini ya uongozi wa HE William Samoei Ruto na HE Abraham Kithure Kindiki,” akasema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!