Maseneta usiku wa Alhamisi walipiga kura kumuondoa ofisini Naibu rais Rigathi Gachagua licha ya kushindwa kutoa ushahidi wa kutosha kwa mashtaka dhidi yake.
Wakili wake alikuwa ameomba kikao kiahirishwe ikadai kuwa Gachagua hangeweza kufika katika seneti kwa sababu alikuwa mgonjwa na alikuwa amelazwa hospitalini. Kulingana na wakili wake Gachagua alikuwa akihisi maumivu ya kifua.
Awali vikao vya seneti vilikiwa vimeahirishwa kwa takriban saa mbili huku spika Amason Kingi akitarajia kuwa Gachagua angejiwasilisha kujitetea na hatimaye kuhojiwa.
Baadaye maseneta waliamua kuendelea na vikao kujadili hoja ya kumuondoa Gachagua licha ya kutokuwepo hatua ambayo ilipelekea mawakili wake kuondoka nje ya seneti.
Jumalililopita thtluthi tatu ya wabunge walipiga kura kumuondoa afisini Naibu rais. Hatua hii ilianzisha mchakato wa kumuondoa Gachagua.
Gachagua ameenda katika hostoria y Kenya kama Naibu wa Kwanza wa rais kuondolewa ofisi kupitia kura ya kutokuwa na imani naye.
Makamu wa rais wa zamani chini ya katiba ya awali hawakuwa na kinga ya sheria na waliteuliwa na kufutwa na rais wakati wote akihisi kufanya hivyo, hali ambayo ilipelekea rais wa zamani Daniel Moi kufuta makamu wake wengi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!