Waziri wa maswala ya ndani Prof. Kithure Kindiki aliteuliwa na rais William Ruto kuwa naibu wake baada ya bunge la seneti kuidhinisha hoja kuhenguliwa kwa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua.
Prof. Kindiki ameidhinishwa na bunge la kitaifa kuwa naibu wa rais baada ya wabunge 236 kupiga kura ya kuidhinisha uteuzi wake.
Wabunge wote waliokuwa katika bunge wakati wa kupiga kura walipiga kura ya kuunga mkono uteuzi wa PProf. Kindiki.
Msomi huyo wa sheria katika chuo kikuu cha Moi jijini Eldoret, aliwahi kuwa seneta wa kaunti ya Tharaka Nithi kwa mihula miwili kuanzia mwaka wa 2013 hadi 2022.
Mbali na kufanya sheria chuoni Moi, Kindiki pia ana cheti cha uzamili ya sheria ya kimataifa aliyohitimu katika chuo cha Pretoria, Afrika Kusini.
Safari ya Prof. Kindiki katika siasa imekuwa ya kufana kwa upande wake kwani pindi tu alichaguliwa kama seneta wa Tharaka Nithi, katika muhula wa kwanza alichaguliwa kama kiongozi wa wengi katika bunge la seneti.
Katika awamu yake ya muhula wa pili bungeni humo, Kindiki alichaguliwa kuwa naibu wa spika wa bunge hilo.
Anapoingia katika nafasi ya naibu wa rais, Profesa Kithure Kindiki anawacha pengo katika wizara ya maswala ya ndani ambapo amekuwa akiongoza tangu kubuniwa kwa baraza la mawaziri katika serikali ya Kenya Kwanza inayoongozwa na rais William Ruto.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!