Mwanasheria maarufu na mwanaharakati wa kisiasa Morara Kebaso ametangaza mipango yake ya kuadhimisha Siku ya Mashujaa inayokuja.

Katika taarifa yake siku ya Alhamisi asubuhi, kiongozi huyo wa chama cha INJECT alitangaza kuwa atazuru Kaunti ya Narok ambako ananuia kushiriki katika shughuli za usafi na elimu ya uraia.

Mwanaharakati huyo kijana aliweka wazi kuwa hataungana na vijana wengine ambao wameashiria nia ya kuhudhuria hafla iliyopangwa na mchekeshaji Eric Omondi siku hiyo hiyo.

“Nasimama na msimamo wangu kwamba mimi sitahudhuria mkutano wa Uhuru Park. Sababu zangu za kutohudhuria ni kwamba sina uhakika, na nina shauku ya mkutano mkutano huo umefadhiliwa. Sijui wafadhili ambao wako nyuma ya mkutano huo, na wanachotaka kukusanya kutoka kwa huo ufadhili,” Morara alisema huku akifafanua sababu ya kutohudhuria hafla iliyopangwa ya Eric Omondi.

 Siku hiyo hiyo rais William Ruto anatarajiwa kuongoza nchi katika kuadhimisha siku ya Mashujaa katika kaunti ya Kwale.

Hii, kulingana na Kebaso, ni sababu nyingine inayomfanya kuwakatisha tamaa watu kufanya mkutano sawia katika bustani ya Uhuru Park.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Kwa rais atakuwa Kwale, nina uhakika kwamba vifaa vya usalama hawataweza kuruhusu kuwa mkutano mkubwa ambao unabishana na ule war ais, haswa mkutano huo uko karibu mita 700 kutoka ikulu. Kwa hivyo itakuwa kama kuchokoza tayari,” alisema.

Mwanaharakati huyo pia aliibua wasiwasi kuhusu hali ya kisiasa ya sasa akibainisha kwamba mchakato unaoendelea wa kumtimua naibu rais Rigathi Gachagua unaweza kuwa na athari kwa siku hiyo.

“Leo kabla ya usiku wa manane, ninashuku kwamba spika wa seneti atatoa notisi ya gazeti, na kabla ya asubuhi rais atakuwa ashatangaza naibu rais mpya. Hali ya kisiasa itakuwa moto sana, hivyo sio wakati mzuri wa mkutano mkutano kuu kwa hivyo mkutano huo unaweza kuchukuliwa na Gachagua ama yeye mwenyewe anaweza kuleta vijana kupitia wabunge wake,” alisema.

Hapo awali, mchekeshaji na mwanaharakati Eric Omondi alikuwa ametangaza hafla iliyopangwa katika bustani ya Uhuru Park Siku ya Mashujaa kusherehekea maisha ya vijana waliofariki wakati wa maandamano ya kuipinga serikali.