KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Oktoba 17.
Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Elgeyo Marakwet, Laikipia, Kirinyaga, na Kiambu.
Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za maeneo ya Dandora na Marururui zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Turesia na Floupar katika kaunti ya Elgeyo Marakwet yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Temu Estate, Cottage Hospital, Jua Kali na Naibor katika kaunti ya Laikipia yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi alasiri.
Katika kaunti ya Kirinyaga, maeneo ya CMI Makutano na Sagana yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Wakati huohuo, Maeneo ya Nazareth Hospital, Membley, Watalaam, Munyu Dispensary, na Magana katika kaunti ya Kiambu pia yataathirika na kukatizwa kwa umeme.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!