Aliyekuwa Mke wa Rais wa Zambia, Esther Lungu, amepoteza mali yake yenye thamani ya mamilioni ya pesa kwa tume ya kupambana na ufisadi nchini humo.
Mke huyo wa rais wa zamani, Edgar Lungu alipoteza jumla ya nyumba za kifahari 15 zenye thamani ya Kwachi milioni 41, sawa na milioni 200 pesa za Kenya, baada ya mahakama kuamua kwamba ilikuwa ni mali kutoka nan a ufisadi, kilisema chanzo kimoja.
Mahakama ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha (EFCC) iliamuru kunyang'anywa kwa orofa zake 15 za kifahari katika State Lodge hadi jimboni.
Mali hizo, zenye thamani ya K41 milioni, zilichukuliwa kuwa zimechafuliwa na mahakama.
Akiandamana na mumewe, Rais wa zamani Edgar Lungu, Mke wa Rais wa zamani hakushangazwa na hukumu hiyo.
"Ilitarajiwa, haishangazi," alisema kwa utulivu kwa mujibu wa ripoti.
Mume wake aliunga mkono maoni yake, akisema, “Tulijua matokeo, na huu ndio uamuzi.”
Uamuzi wa EFCC, uliotolewa kwa faragha katika Mahakama ya Juu, ulihitimisha kuwa Esther Lungu alishindwa kutoa uthibitisho wa vyanzo vya mapato kwa ajili ya ujenzi wa mali hizo, licha ya utetezi wake kuwa ni mali ya ndoa.
Timu yake ya mawakili, ilitangaza mipango ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Katika utetezi wake, Bi. Lungu alishikilia kuwa DPP alikiuka katiba kwa kujaribu kunyakua mali zake bila kwanza kuthibitisha hatia yake kupitia kesi.
Alisisitiza kuwa orofa hizo ni sehemu ya mali yake ya ndoa, iliyoendelezwa na mumewe, Rais wa zamani Edgar Lungu.
DPP alipinga kwa hoja kwamba Bi. Lungu anapaswa kutoa ushahidi wa maandishi, kama vile taarifa za benki, ili kuthibitisha madai yake kwamba mumewe ndiye aliyefadhili ujenzi wa majengo hayo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!