Mwanaharakati wa elimu ya kiraia, Morara Kebaso amevutia hisia mseto katika mtandao wa X baada ya kuomba Wakenya na wahisani wema kujitolea katika kumchangia hela za kununua kompyuta.
Kebaso, ambaye awali alitangaza kuanzisha biashara ya kuuva nguo zenye chapa na nembo ya chama chake cha INJECT alirudi kwenye jukwaa hilo akiweka wazi nia ya ofisi yake kuwa na kompyuta na vichapishi kwa ajili ya kazi za kiraia.
Baada ya watu kuibia maswali kuhusu michango yake ya kila mara, Kebaso alijitetea akisema kuwa yeye kama kiongozi ni sharti abuni njia za kupata rasilimali za kuendesha shughuli zake kwa ajili ya umma.
“Lazima nitafute njia za ubunifu za kuongeza rasilimali. Kama kiongozi, ni kazi yangu kufikiria jinsi mabadiliko tunayotaka yanaweza kupatikana. Kwa hivyo naomba ushirikiane nami katika hilo,” Kebaso aliomba.
“Infact hapa ni Namba ya Mpesa, wekeni kakitu tunataka kununua kompyuta tatu na printer kubwa mbili. Haya yatatumiwa na timu ya kisheria ya mawakili wa kujitolea ambao watakuwa wakiwasilisha kesi mahakamani kusaidia Wakenya,” aliongeza.
Kebaso alisisitza kwamba hakuna baya lolote vanalofanya kwani kila mchango anaoupata huwa anatoa sasisho ya jinsi hela hizo zinavyotumika.
Alisema kwamba yeye ni macho na masikio ya Wakenya na kila kitu anachofanya kinafadhiliwa na Wakenya wengine akisema hawajuani na wala hawajawahi kutana nao.
“Ninafadhiliwa kwa asilimia 100 na Wakenya kwa Mpesa. Wengi wao sijawahi kukutana nao. Lakini siwezi kuwaomba michango kila siku kwa sababu wakati fulani watakuwa wamechoka,” alifafanua.
Kuomba mchango huu kunajiri wiki moja tu baada ya kurudi katika mtandao huo akiomba kuchagiwa ili kuongeza usalama wake.
Kebaso aliomba kuongezewa usalama baada ya kushambuliwa na vijana katika ukumbi wa Bomas wakati wa hadhara ya kutoa maoni kuhusu kung’atuliwa ofisini kwa naibu rais, Rigathi Gachagua.
Katika video, Kebaso alionekana akijaribu kujinasua kutoka kwa zogo hilo ambalo alikuwa anarushiwa viti.
“Ninaomba Wakenya wa nia njema waniunge mkono katika kuimarisha miundombinu yangu ya usalama na wafanyakazi,” aliomba mnamo Oktoba 7.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!