KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Septemba 16.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, Kiambu, Nyeri, Kisumu, na Migori.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Eastleigh, V Club, na St Bhakita zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Kamiti Road, Ruturo, Gitaru, Muthure, Nyathuna, Ngethu Road, na Naivasha Road zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Ndunyu, Gitugi na Ihithe katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Kisumu, sehemu za maeneo ya Angira na Kibos Sugar zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Awendo na Ranen katika kaunti ya Migori pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!