YouTuber Diana Marua amelazimika kuomba msaada kwa wafuasi wake kwenye mtandao wa kijamii baada ya mwanawe mdogo kumfokea vikali kama mwana rika nwenza.


Marua alichapisha video fupi kwenye Instagram akionyesha wakati binti yake mdogo, Malaika Bahati akimfokea na kumtaka kuacha kuingilia maisha yake.


Alijaribu kumshika binti huyo aliyefikisha umri wa miaka miwili hivi majuzi, lakini kwa hali ya kushangaza, binti huyo alimgeukia kwa fujo na kumuuliza ‘shida yako ni nini?’ huku akimtaka kumkoma.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


“Shida yako ni gani?” Malaika alimfokea mama yake aliyeachwa katika hali ya mshangao.


Baadae, Diaa alimuuliza binti yake kwa nini anamfokea hivo na binti huyo akakataa kukiri kama amemfokea, akisema, “sijakufokea”.


Mama mtu alijaribu kumshurutisha mtoto huyo kuomba radhi kwa kusema samahani lakini mtoto huyo aliyeonekana kughadhabika na uwepo wa mamake karibu naye alikataa katakata kuomba msamaha.


Ilimbidi Diana atafute ushauri kwenye mitandao kuhusu ni jinsi gani anaweza kuishi na mtoto huyo ambaye tayari ameanza kuonyesha jeuri akiwa katika umri mdogo.


“Unaweza kufikiria kuulizwa una shida gani na mtoto ambaye ana miaka 2 tu??? ?️ @malaika_bahati ananiambia kwa Ujasiri kuwa mimi ndiye ninayepiga kelele, sio yeye ??? Huyu Nimfanyeje? Mmmhh!!! Mtu anishike,” Marua aliomba.