Mwanaharakati wa kutoa elimu ya kirais, Morara Kebaso ameanzisha biashara ya kuuza mavazi yenye nembo ya chama chake kipya cha INJECT.
Read Also
Kebaso, kupiotia kitandazi cha X, aliweka wazi kwamba ameanza harakati za kukitangaza chama hicho kwa umma cha INJECT, wiki chache baada ya kukisajili rasmi.
Enjoying this article?
Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans
"Nguo za INJECT ziko hapa, shili ngi 2500 kwa kila moja,' Kebaso aliandika.
"Nguo hizi zimeundwa ili kuonyesha chapa ya humu nchini Kenya, ubora ni wa kiwango kizuri ndio maana inagharimu 2,500.Pamba safi, UNISEX kwa wanaume na wanawake,' alizipigia debe.
Mwanaharakati huyo alisema kwamba huu ni mkakati wa kukusanya rasilimali zaidi kwa ajili ya kuendesha chama hicho ambacho ni kipya zaidi humu nchini.
"Huu ni mkakati wetu kwa ajili ya kukusanya rasilimali za kuendesha chama. Pesa zote zitatumika katika kujenga harakati zenye nguvu zaidi na shughuli z ufadhili kama vile kesi za mahakama zenye maslahi ya umma," aliongeza.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!